Na:
Hashim Jumbe
Ujumbe wa Kamati ya Mifugo kutoka Manispaa ya Ilala
ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Imelda Samjela umefanya ziara ya mafunzo katika
Manispaa ya Sumbawanga, na kutembelea machinjio ya SAAF, machinjio ya Manispaa
ya Sumbawanga na viwanda vidogo vya ngozi(SIDO).
Ziara hiyo iliwaambatanisha Madiwani wa Manispaa ya
Ilala, Watendaji na Maafisa Wafawidhi wa machinjio ya Vingunguti na Ukonga,
walipata pia fursa ya kutembelea hifadhi ya chakula NFRA na sehemu ya mnada
wa n’gombe KAMITA.
Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bw. Jesse Mkumbo akiwakaribisha Wajumbe wa
Kamati ya Mifugo kutoka Manispaa ya Ilala katika Ofisi ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Sumbawanga
|
Wajumbe wa Kamati ya Mifugo kutoka Manispaa ya Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Sumbawanga mbele ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga
|