Lengo la zoezi hili
ni kupata taarifa na takwimu sahihi za wakazi wetu na wafanyabiashara wote ndani
ya Halmashauri ya manispaa ya Ilala ambazo zitatusaidia kuboresha huduma kwa
wananchi wetu kutokana na idadi na mahitaji ya kila eneo.
Zoezi hili linaanza
rasmi leo tarehe 08/04/2015 hadi tarehe
08/07/2015 na litahusisha maeneo yote kuanzia katikati ya mji na meneo ya
pembezoni.
Katika kipindi hicho
watumishi wa Manispaa pamoja na waajiriwa wapya watapita maeneo yote kwa ajili
ya kukusanya taarifa mbali mbali za kodi, tozo, leseni na malipo ya aina zote
ikiwemo ushuru wa mabango ambapo mabango yote ndani ya Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala yatapimwa upya ili kujiridhisha na vipimo vya awali.
Maeneo mengine
yatakayohusika ni ushuru wa masoko pamoja na ushuru wa kuzingira kwenye maeneo
ya ujenzi.
Tunawaomba wananchi
wetu na wafanyabiashara wote ndani ya manispaa ya Ilala kuwapa ushirikiano
wafanyakazi wetu watakaopita katika maeneo yao. Pia tunawaomba wamiliki wa
majengo kuacha taarifa zote muhimu ili kufanikisha zoezi hili; taarifa muhimu
kwa wamiliki wa nyumba ni;
Ø Jina
kamili la mmiliki
Ø Stakabadhi
za malipo ya mara ya mwisho kama zipo
Ø Makadirio
ya malipo yaliyofanywa na Manispaa kama yapo.
Endapo kutajitokeza tatizo
lolote tunawaomba wananchi na Wafanyabiashara kuwasiliana na ofisi za Watendaji
wa Kata au Mitaa katika maeneo yao ili kupata ufafanuzi zaidi.
Pamoja na zoezi hili
shughuli zote za kukusanya mapato, ulipaji wa tozo mbali mbali
na ukataji wa leseni za biashara zitaendelea kama kawaida.
Imetolewa na,
Isaya
M.Mngurumi
Mkurugenzi
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala