Afisa
Mwandikishaji Manispaa ya Ilala anawatangazia wenye sifa kujitokeza kuomba
nafasi ya kazi ya kuwa BVR OPERATORS AU MWANDISHI MSAIDIZI kwenye zoezi la Uboreshaji
wa Daftari la kudumu la Wapiga kura.
Sifa za Mwombaji
i.
Awe
ni Raia wa Tanzania
ii.
Awe
ni Mkazi wa Manispaa ya Ilala
iii.
Awe
anajua kusoma na kuandika
iv.
Awe
na Elimu ya Sekondari na kuendelea
v.
Awe
na Elimu ya kiwango cha cheti na kuendelea ya matumizi ya Kompyuta
vi.
Awe
ni Mkazi wa Kata anayoombea kufanya kazi
Jinsi ya kutuma maombi
i.
Barua
ya maombi iandikwe kwa mkono ikiwa na anuani kamili ya mwombaji na kuambatanishwa
na vivuli ya vyeti.
ii.
Mwombaji
ataje Kata anayoishi ambayo anaombea
kufanya kazi hiyo
iii.
Barua
za maombi ziwasilishwe Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala (Afisa
Mwandikishaji) iliyopo katika makutano ya Barabara
ya Mission na Sokoine kwa kutumia anuani ifuatayo;
Afisa
Mwandikishaji,
Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala,
1
Mtaa wa Mission,
S.L.P
20950,
11883-Dar
es Salaam.
N.B Siku
ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 19/06/2015 saa 9:30 alasiri.
Limetolewa na,