Na: Tabu Shaibu
Zoezi linaloendeshwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala la
ukusanyaji wa takwimu za mapato lililoanza tarehe 08/04/2014 limekamilika rasmi
tarehe 8/07/2015. Zoezi hili lilihusisha takwimu za Majengo, Leseni za
Biashara, Mabango, Vibali vya Kuzingira na Vibali vya kuingiza Makontena Mjini pamoja na Wafanyabishara wa masoko.
Manispaa iliajiri kwa
muda vijana takribani 300 waliokuwa wakikusanya Takwimu hizo chini ya Usimamizi
wa Maafisa wa Manispaa.
Akiwaaga vijana walioshiriki zoezi hilo kwenye Ukumbi wa
Mikutano wa Arnatoglou, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bwana Isaya Mngurumi
aliwashukuru kwa kuweza kufanikisha zoezi hilo na kuwaeleza kuwa limeifanya Halmashauri
yake kupiga hatua katika mpango wa kuwa na Database
sahihi ingawa wapo waliopinga zoezi hili lililopoanza. Mngurumi aliendelea kueleza kuwa, ushirikiano
uliokuwepo baina yao na Maafisa wa Halmashauri na kwa kila mmoja kujituma
katika nafasi yake kumewezesha upatikanaji wa takwimu kwa baadhi ya Kata.
“Awali zoezi hili lilitakiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu. Hata hivyo changamoto zilizojitokeza zimesababisha kazi hii kutokamilika na sasa Halmashauri itaendelea tena na zoezi hili kwa kipindi cha miezi mitatu na tayari iliyokuwa Kamati ya Fedha ya Madiwani imetoa kibali cha zoezi hili kuendelea”. Alisema Mngurumi.
|
Mratibu
wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mapato ‘BRN- Mapato’ Manispaa ya Ilala
Bwana Francis Luambano akitoa ufafanuzi wakati wa kuhitimisha awamu ya kwanza
ya zoezi hilo.
|
|
|
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Isaya
Mngurumi akizungumza na Vijana walioshiriki zoezi la ukusanyaji wa takwimu za
mapato ‘BRN-Mapato’ wakati wa kufunga awamu ya kwanza ya zoezi hilo
|
|
Mshiriki wa awamu ya kwanza ya zoezi la ukusanyaji
wa takwimu za mapato akizungumza wakati wa kufunga awamu ya kwanza ya
ukusanyaji wa takwimu za mapato
|
|
Mmoja wa Washiriki wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu
za mapato, akitunukiwa cheti cha ushiriki na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
Ndugu Isaya Mngurumi
|