Na: Hashim Jumbe
Ni takribani miezi nane sasa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Mhe. Paul Makonda aweke jiwe la msingi kwenye ujenzi wa hospitali kubwa na ya kisasa itakayotoa huduma ya Mama na Mtoto inayoendelea kujengwa Chanika, Manispaa ya Ilala, siku ya jana ya tarehe 6 Disemba, 2016 Mhe. Makonda amerudi tena na kukagua ujenzi huo namna unavyoendelea.
Ujenzi wa hospitali ya Mama na Mtoto ya Chanika unafadhiliwa na Serikali ya Watu wa Korea Kusini (KOICA) ulianza mwezi Februari,2016 chini ya Mkandarasi aitwaye 'China Hunan Engineering Construction Company' na unategemea kukamilika ndani ya miezi 12, na gharama zake ni Dola za Kimarekani Milioni 4 sawa na Tshs. Bilioni 8.8 za Kitanzania.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi, Mhe. Paul Makonda alifurahishwa na hatua ya ujenzi huo ilipofikia, ambapo kwa mujibu wa Mkandarasi anayesimamia ujenzi huo amesema ujenzi huo umekamilika kwa 80% na mpaka kufikia mwezi Februari, 2017 ujenzi huo unatarajiwa kukamilika kwa 100%
Ujenzi wa hospitali hiyo ni ahadi ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuboresha huduma za afya kwa Wananchi wake, na hospitali hiyo inatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa