MANISPAA YA ILALA VINARA UMITASHUMTA MKOA WA DSM KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO

Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imefanikiwa kushinda Ubingwa wa Jumla wa mashindano ya UMITASHUMTA kwa Mkoa wa DSM kwa mwaka 2017, ikiwa ni mara ya pili mfululizo.  Ubingwa huo unafuatia ushindi wa Mpira wa Miguu kwa Wavulana, ushindi wa Mpira wa Miguu kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum na ushindi wa jumla wa riadha.

Mbali na ushindi huo, Wanafunzi wa Manispaa ya Ilala wameongoza pia kwenye idadi ya Wanafunzi wanaokwenda kuunda timu ya Mkoa wa DSM kwa ajili ya Mashindano ya UMITASHUMTA Ngazi ya Taifa yanayotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza katikati ya mwezi huu. Idadi ya Wanafunzi toka Manispaa ya Ilala ni 30 kati ya Wanafunzi 97 huku Walimu na Waratibu toka Ilala wanaokwenda kwenye timu ya Mkoa ikiwa ni Wanne.
Maandamano ya Wanafunzi, Walimu na Wakufunzi walioshiriki UMITASHUMTA Mkoa wa DSM, yakipita mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa kilele cha mashindano hayo yaliyoendeshwa kwa siku tano kwenye viwanja vya Uhuru na DUCE






Mgeni Rasmi kwenye ufangaji wa mashindano hayo ambaye alimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa DSM, Bw.Kiduma Mageni akiongea na washiriki wa UMITASHUMTA kwa mwaka 2017 pamoja na kutoa salamu za Katibu Tawala Mkoa wa DSM, Bi. Theresia Mmbando











Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Bi. Elizabeth Thomas akikabidhiwa kombe la Ushindi wa Jumla UMITASHUMTA Mkoa wa DSM na Mratibu wa UMITASHUMTA Wilaya ya Ilala


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi