Na: Hashim Jumbe
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko, leo amewaongoza Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kutembelea Kampuni ya ITV inayoendesha kituo cha habari cha ITV, Radio One, Capital Radio, Capital Television, EATV na East Africa Radio.
Katika ziara hiyo, ujumbe kutoka Manispaa ya Ilala ukiongozwa na Mstahiki Meya ulijionea namna vyumba vya habari vinavyofanya kazi kuanzia wanavyopokea habari, wanavyoziandaa hadi kutangazwa kwake na uhifadhiwaji wa habari hizo.
Aidha, mbali na lengo la kujifunza kwenye ziara hiyo, lakini pia ziara hiyo imetengeneza fursa ya mwanzo wa mahusiano mazuri kati ya Manispaa ya Ilala na Kampuni ya ITV, ambayo inafanya kazi ya kutoa habari za kuelimisha Umma pamoja na kuhabarisha.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Kampuni ya ITV |
Wageni toka Manispaa ya Ilala wakiongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Charles Kuyeko walipotembelea studio za Capital radio |