Na: Hashim Jumbe
Mradi wa Maendeleo kwa Mji wa Dar-es-Salaam 'Dar-es-Salaam Metropolitan Development Project' (DMDP) ni mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa msaada wa Serikali za Mitaa (LGSP2) amabao utaimarisha fedha, kugawa Mamlaka, kuboresha uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za Serikali za Mitaa na kuboresha usimamizi wa mifumo ya uhamisho kati ya Serikali
Mradi wa DMDP unalenga kuimarisha mifumo ya usimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Jiji la Dar-es-Salaam ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi kwa wakati na mradi huu umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, yaani kuanzia mwaka 2015-2020.
Manispaa ya Ilala ni miongoni mwa Halmashauri tatu zilizopo Dar-es-Salaam ambazo zipo kwenye utekelezaji wa mradi wa DMDP, ambapo mradi huu unatekelezwa katika vipengele vinne. Utekelezaji wa vipengele hivyo ni kama ufuatao:
1) Eneo la Miundombinu;
kwenye kipengele hiki, mradi utagusa maeneo mawili, ambayo ni;
a) barabara za mitaani, ambapo kwa Manispaa ya Ilala zitajengwa barabara zenye urefu wa kilomita 13
b) uboreshaji wa miferiji ya maji ya mvua
2) Uboreshaji wa makazi holela;
katika eneo hili kutakuwa na uboreshaji kwenye barabara, mifereji, masoko, vyoo vya Umma, vizimba vya taka na magari ya kukusanyia taka na kata zitazonufaika na mradi ni Kata ya Kiwalani ambayo itakuwa na barabara yenye urefu wa kilomita 14, Kata ya Ukonga itakuwa na barabara ya kilomita 6 na Kata ya Gongolamboto kilomita 4.
3) Kuimarisha na kujenga uwezo wa Taasisi;
katika eneo hili, mradi utahusika na ujengaji wa uwezo kwa Watumishi wa Manispaa ya Ilala, kuimarisha mfumo wa ukusanyaji mapato.
4) Kutoa msaada wa utekelezaji wa mradi;
katika eneo hili kampuni zitakazotoa msaada wa utekelezaji ni UWP, Lea Associates

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Nitu Palela akitia saini kwenye mkataba wa utekelezaji wa mradi wa DMDP, huku akishuhudiwa na Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Bw. Bonaventure Mwambaja |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe.Charles Kuyeko aliye upande wa kulia akisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa DMDP pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela |