Na: Hashim Jumbe
Mradi huo wa uboreshaji na upendezeshaji wa Mtaa wa Samora umeratibiwa na Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala pamoja na Shirika la Maendeleo toka Nchini Japan 'JICA'.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo toka Japan 'JICA' leo wameandika historia mpya kwenye Jiji la DSM, historia ambayo inaweza isifutike miongoni mwetu kwa miaka dahali, historia ya kuiona DSM mpya iliyopangika na yenye maeneo ya vivutio na mahala pakupumzikia Wananchi wake.
Katika harakati za kuipendezesha DSM na kutaka ionekane kama Miji mingine mikubwa iliyoendelea Duniani, Mtaa wa Samora umekuwa mfano 'pilot project' kwa namna gani DSM mpya inavyotakiwa kuonekana na leo hii Mkuu wa Mkoa wa DSM, Mhe. Paul
Makonda amezindua rasmi Mradi wa Maboresho ya Mtaa
wa Samora.