MUONEKANO WA SOKO LA SAMAKI FERI BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI WA MIUNDOMBINU

Na: Hashim Jumbe
Ni miaka 17 sasa tangu soko la samaki feri lijengwe, soko hilo la kimataifa ni maarufu kwa uuzwaji wa samaki wanaovuliwa kutoka bahari ya Hindi na kuingia sokoni hapo kwa ajili ya kuuzwa, samaki hao huvuliwa kutoka Dar es Salaam na maeneo ya jirani kama vile Bagamoyo, Pemba, Mafia,Kilwa na kwengineko.

Katika kulifanya soko hilo linabaki katika uimara na muonekano ulio nadhifu na wa kuvutia, Bodi ya Soko la Samaki feri wamefanya ukarabati mkubwa wa miundombinu katika mfumo wa maji taka ambao ulishaanza kuchoka, katika ukarabati huo Jumla ya Shilingi Milioni 36.8 zimetumika.

Ukarabati mwengine uliofanyika sokoni hapo ni mfumo wa umeme ambao umegharimu Jumla ya Shilingi Milioni 35.7. Aidha pamoja na ukarabati wa miundombinu, lakini pia majengo 8 ya sokoni hapo yameweza kupakwa rangi na gharama iliyotumika ni Jumla ya Shilingi Milioni 42.5

Kazi nyengine zilizofanyika sokoni hapo ni ujenzi wa Karakana iliyogharimu Shilingi Milioni 54.5, Ujenzi wa Jengo la Mamalishe  'Zone 8 A' kwa gharama ya Shilingi Milioni 26.6 na ujenzi wa 'Zone 8 B' sehemu ya wauzaji samaki na gharama zake ni Shilingi Milioni 14.1

Ukarabati wa miundombinu, kupaka rangi pamoja na ujenzi uliofanyika sokoni hapo umetokana na fedha za makusanyo kutoka kwenye soko hilo, ambapo wameweza kutumia 'force account' kufanikisha ukarabati na ujenzi huo.

Muonekano mpya wa Soko la Kimataifa la Samaki Feri baada ya kufanyiwa ukarabati.





Ujenzi wa Jengo la 'Zone 8A' kwa ajili ya Mama Lishe sokoni hapo





Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi