Wiki ya Usafi wa Mazingira yazinduliwa; Walimu wa afya mashuleni na Wafanyakazi wa Afya ya Jamii wapata mafunzo

 

Na; Shamimu Msuya

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imefanya mafunzo kwa walimu wa Afya, CHW (Community Health Workers) na maafisa Afya wa Wilaya kuadhimisha wiki ya usafi na siku ya choo duniani.

Mafunzo hayo yametolewa kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Manispaa ya Ilala chini ya mdau wake AMREF kwa lengo la kuelimisha jamii hasa wanafunzi mashuleni juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira, kujikinga na magonjwa na matumizi sahihi ya choo




.Aidha, Afisa Afya wa Manispaa ya Ilala Bi. Esther Ng’ang’ano ameeleza kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa siku nne (04) kwa shule 19 kutoka kata 6 zinazofanyiwa maboresho na AMREF ambapo tarehe 16 – 18 Novemba, 2020 ni siku za mafunzo kwa walimu wa afya, CHW pamoja na maafisa afya yakiambatana na utoaji wa elimu ya afya mashuleni na kilele ni tarehe 19 Novemba, 2020 ambapo kutakuwa na hafla fupi na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi watakao wasilisha vizuri elimu waliyopata.








Sambamba na hayo, Afisa mradi usafi wa mazingira na afya (AMREF) Bi. Annastazia Lutatina ameeleza kuwa wanashirikiana na Manispaa ya Ilala kama mdau katika kuadhimisha wiki ya usafi na siku ya choo duniani kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya usafi wa mazingira, kunawa mikono na matumizi sahihi ya choo kwa wananchi hasa wanafunzi mashuleni na wamechagua kata 6 ambazo zinafanyiwa maboresho na AMREF kupitia mradi wake wa HBC (Hygiene and Behavior Change) unaofanyika kwenye Manispaa ya Ilala.



                  Afisa mradi usafi wa mazingira na afya (AMREF) Bi. Annastazia Lutatina


Hata hivyo, Bi. Annastazia amemalizia kwa kusema kuwa, lengo kuu la kufanya mfulilizo wa shughuli hizo za kijamii ni kuelimisha jamii na kusaidia kufufua Club za afya mashuleni ili kutokomeza maambukizi ya magonjwa ya mlipuko na kujenga tabia ya usafi kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi