Na Mariam Hassan
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Amos Makalla leo tarehe 22/06/2021 ametembelea Soko la Machinga Complex na kujionea shughuli nzima za uendeshaji wa biashara zinavyofanyika, Akiwa katika eneo hilo Mkuu wa Mkoa ameweza kusikiliza kero mbali mbali kutoka kwa wamachinga wanaofanya biashara zao katika eneo hilo.
Mhe. Makalla akizungumza na waandishi wa habari alisema kuna haja ya kutembelea Machinga Complex mara kwa mara kujua maendeleo yanayoendelea katika soko hilo ili kuweka uhusiano wa karibu na wamachinga hao, biashara zisifungwe kutolewe mda wa kuongea na kuwepo na dawati la kudai ili kukaa kujadili ni jinsi gani madeni yote yanalipwa ili kuweza kupata hizo pesa kwa ajili ya kuongeza mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla akizungumza na wafanyabiashara wa Soko hilo |
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Ng’wilabuzu Ludigija amesema “Wataanza na wafanyabiashara walioshindwa kulipa vizimba vifunguliwe na kukaa na wafanyabiashara kuona namna jinsi watakavyolipa hizo hela, na pia watashughulikia swala la kuchagua uongozi ili wakija kusikiliza kero wakutane kwanza na uongozi. Watakaa na viongozi wa Wamachinga kupanga utaratibu mzuri wa wamachinga ambao hawana eneo la kufanya biashara wapate sehemu ya kufanya biashara na pia wataangalia mda wa kufanya biashara kwa kukaa na jeshi la polisi kujadiliana”
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla wakijionea shughuli zinazoendelea katika Soko hilo |
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Ndg. Jumanne Shauri amesema “watafanya mpango mpya wa kuwapanga wafanyabiashara waliopo eneo hilo ili biashara zinazofanyika sehemu nyingine zisifanane, nimemuelekeza meneja wa soko awasiliane na Tanesco ili wawekewe mita zao na kuepuka kuwa na mita moja jengo zima”
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akitembelea Soko la Machinga Complex lililopo Ilala |
Pia Mkurugenzi wa Jiji ameelekeza magari saba yakachukue takataka katika soko hilo na kutatengenezwa miundombinu kwa ajili ya kuepusha maji kutuama katika soko hilo.