Mkuu wa Idara ya Mazingirana udhibiti wa Taka ngumu Bw.Rajabu Ngoda akikata utepe katika eneo lililotayarishwa kwaajili ya ujenzi wa tank la maji Gereza la Maabusu Segerea |
Mfuko wa maendeleo ya
jami(TASAF) kupitia Halmashauribya Jiji la Dar es Salaam leo August 25, 2021 wamezindua mradi wa
ukirabati wa miundombinu ya maji safi na salama pamoja na uwekaji wa tank la liter Laki 1 katika ukumbi wa Gereza la Maabusu Segerea lengoblikiwa ni
kusaidia upatikanaji wa maji safi na slama katika Gereza hilo.
Akizungumza katika Hafla
hiyo Mratibu wa TASAF - Halmashauri ya
Jiji la Dar es salaam Bi. Marcella Msawangwa amesema kuwa mfuko wa maendeleo ya
jamii(TASAF) kwa awamunya Tatu ambao
ulizinduliwa kwa lengo la kunusuru kaya maskini katikansekta ya Afya, Elimu
pamoja na kusidia jamii kutekeleza miundombinu ya Maji na barabara umeona
siobudi kusaidia upatikaji wa maji safi na salama kwa Gereza la Maabusu Segerea
ili kuweza kutatua changamoto ya maji katika Gereza hilo.
Aidha Bi. Maricella ameeleza
kuwa mradi huo ambao unatarajiwa
kukamilika Desemba, 2021 utagharimu takribani shillingi million 197 ambapo mradi huo utaanza kutekelezwa mara baada ya mafunzo ya
siku tatu (3) ambayo yalizinduliwa katika hafla na kuanza rasmi Agust 25 hadi
Agust 27, 2021 hivyo baada ya mafunzo hayo kukamilika mradi utaanza kutekelezwa kwani
utaratibu wa manunuzi pamoja na kupata local fundi ushaanza kufanyika.
"Ni matumaini
yangu kuwa kwakua tushatangaza tender za kupata local fundi mara baada ya
mafunzo tutaanza utekelezaji wa mradi ambao unatarajiwa kukamilika Desember
2021 kwani fedha ya kutosha ipo hivyo hakutakua na changamoto ya kifedha
itayokwamisha mradi huu".alieleza
Bi.Marcella.
Vilevile, Akizungumza kwa
niaba ya Mkuu wa Gereza la Maabusu Sagerea Mrakibu wa Maabusu Athanas Ndowano
ameeleza kuwa tatizo la maji katika Gereza hilo ni kubwa ukilinganisha na
mahitaji ya watu waliopo maabusu hivyo ujio wa mradi huu ni ukumbozi mkubwa kwa
Gereza la Maabusu Segerea pamoja na wananchi wa mtaa wa Mgombani na Kata za
jirani ambao wataweza kufaidika na mradi huu.
"Tatizo la maji
lilikua kubwa hivyo tunatoa shukrani zetu kwa Mradi wa maendeleo ya Jamii
(TASAF) pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
kuona tatizo la Magereza kama sehemu yao hivyo tunaahidi kufanya kazi kwa
uweledi mkubwa kama ilivyokusudiwa".alisema Mkaribu Athanas.
Sambamba na hilo akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam Comisioner msaidizi wa
Magereza Focus Ndabita ameahidi
kuwa watasimamia kamati ya ujenzi wa
mradi huo na watahakikisha wanafuatilia kwa ukaribu na weledi mkubwa ili ujenzi
huo uweze kukamilika kwa wakati.
Akifungua mafunzo pamoja na kuzindua mradi huo
wa ukarabati wa miundombinu ya maji safi na salama pamoja na ujenzi wa tank la
lita Laki 1 kwa niaba ya Mkurugunzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw.
Rajabu Ngoda amesisitiza ushirikishwaji
wa wananchi katika utekelezaji wa mradi huo pamoja na utunzaji wa nyaraka ili
hata ifikapo kipindi cha Mwenge wa Uhuru 2022 mradi uweze kuwekewa jiwe la
Msingi bila dosari yoyote.