Na: Judith Damas
Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 02 Novemba, 2021 wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 ulioanza Julai hadi Septemba 2021.
Wakiwa
kwenye ziara hiyo, kamati iliweza kutembelea na kukagua miradi minne
(4) ikiwemo ujenzi wa Barabara ya nje katika machinjio ya vingunguti na
ujenzi wa mabucha ya nyama vingunguti, ujenzi wa paa la Machinga
Complex pamoja na stendi ya daladala ya Kinyerezi iliyopo chini ya mradi
wa DMDP.
Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inayoongozwa na Mhe. Sultan Salim ikikagua ujenzi wa Barabara ya nje katika Machinjio ya kisasa ya Vingunguti
Aidha,
ujenzi wa barabara ya nje katika machinjio ya vingunguti uliogharimu
takribani shilingi Milioni 264 kazi ikiwa kwenye hatua ya ukamilishaji
huku ujenzi wa mabucha wenye gharama ya shilingi Milion 197.7 ujenzi
ukiwa unaendelea.
Kwa upande mwingine kamati iliweza kutembelea ujenzi wa paa katika Soko la Machinga complex ambapo mradi umeshakamilika na biashara zinaendelea.
Naye,
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Sultan Salim akifanya majumuisho ya
ziara hiyo amesema, "Leo tumetembelea baadhi ya miradi inayosimamiwa na
kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na
utekelezaji huo japo kuna marekebisho madogomadogo yakukamilisha
hususani katika stendi ya kinyerezi"