Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yaendelea kutekeleza shughuli za Lishe bora na Salama katika Jamii

 Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imefanya kikao cha Robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2022 kilichofanyika leo tarehe 26, Mei 2022 katika ukumbi wa mkutano wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kupitia taarifa ya utendaji kazi na utekelezaji wa afua za lishe za Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, Afya, Mifugo, Maji, Maendeleo ya Jamii na Vijana, Elimu Msingi na Sekondari, MDH pamoja na vyombo vya habari  wa Kamati hiyo.

Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

 

Akiongoza Kikao hicho cha Lishe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam  Afisa Uhusiano wa Jiji la Dar es Salaam Bi.Tabu F. Shaibu ameeleza kuwa Kamati ya Lishe ni Kamati muhimu inayotekeleza na kusimamia ulaji na uandaaji wa lishe bora kwa afya za  Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kilimo, Umwagiliaji na Ushiriki  kwa niaba ya Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Vernice  Malisa alieleza kua Idara imeweza kuhamasisha Wakulima 484 waliopo kwenye mabonde ya Kata za Msongola, Zingiziwa, Chanika, Kivule, Buyuni, Ukonga, Gongolamboto na Kitunda kuvuna maji  ya mvua kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa mboga mboga  ifikapo June, 2022.

Aidha Bi. Malisa aliendelea kueleza kuwa katika kuhakikisha Wananchi wanapata mboga mboga salama  Idara imeendelea kutoa elimu na kuhamasisha kilimo cha Magorofani ambacho hutumia eneo dogo katika uzalishaji kwani  mbogamboga hupandwa  katika mifuko ya Salfet na makopo ambayo hayachukui nafasi kubwa ambapo wakulima waliweza kuhamasishwa kuhusu matumizi ya Teknolojia ya kilimo bora ili kuongeza upatikanaji wa chakula cha kutosha chenye lishe bora na Salama kwa mlaji kupitia Shamba Darasa MOJA la mboga katika kiyuo cha Kata cha Rasilimali Kilimo Kinyamwezi.

Kwa upande wake Kaimu Mratibu Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bibi. Neema Mwakasege alieleza kuwa Kamati  itafanya ziara ya mafunzo ya kilimo katika kituo cha Shamba DARASA MOJA la mboga katika Kituo cha Kata cha Rasilimali KIlimo Pugu Kinyamwezi ili kujifunza kilimo cha Magorofani na namna bora ya utayarishaji wa upandaji mbogamboga kwa njia salama ambapo kamati itakua na jukumu la kuelimisha jamii ikijikita katika shule za msingi na sekondari ili wanafunzi hao waweze kufikisha Elimu hiyo katika Jamii inayowazunguka.

Kaimu Mratibu Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bibi. Neema Mwakasege akizungumza jambo

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi