Watumishi wa Jiji la Dar es Salaam watakiwa kuwa waadilifu

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuwa wazalendo na waadilifukatika kuwatumikia wananchi na Serikali yao kwa ujumla.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo Leo tarehe 14, Disemba 2022 katika kikao maalum cha kusikiliza kero za watumishi wa Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Arnatoglo.

Kutoka kushoto: Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Charangwa Makwiro, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Ando Mwankunga

 

Aidha, amewataka viongozi kufanya kazi kwa ukaribu na watumishiili kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za Utumishi wa Umma. Amesema, "Ninawaomba sana watumishi wenzangu tujitume,ilikuhakikisha tunafikisha huduma stahiki na bora kwa wananchi Mhe. Rais anamatumaini makubwa na sisi, hivyo tusimuangushe."

Pia ametoa rai kwa watumishi wote kuwa Serikali haitawavumilia watumishi wote wanaofanya kazi kwa mazoea na wote watakaobainika kuihujumu Serikali kwa namna moja au nyingine hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuondolewa kwenye mfumo wa ajira.

Sambamba na hayo amewaomba watumishi kufanya kazi kwa ukaribu na Taasisi nyingine za Umma kwani wote ni watoto wa nyumba moja ambayo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni lazima wafanye kazi kwakushirikiana ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali yanafikiwa kikamilifu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi