Watumishi Jiji la DSM wamzika Dada Nuru Sigera

Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 22 Januari, 2024 wameshiriki katika shughuli za mazishi ya Muhasibu aliyekuwa Meneja wa Chanzo cha Mapato ya Faini za Mazingira, Marehemu Nuru Sigera.


Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la DSM, Bi. Benadetha Mwaikambo alisema "Dada Nuru Sigera alianza kusumbuliwa na changamoto ya kiafya miezi mitatu iliyopita na tarehe 08 Januari, 2024 alilazwa kwenye Hospitali ya Regency ambapo alikuwa anapatiwa matibabu hadi umauti ulipomfika tarehe 21 Januari, 2024"


Aidha, Marehemu Nuru Sigera alihamia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, tarehe 16 Januari, 2014 na kuhudumu kwa miaka 10 mpaka umauti ulipomkuta

'Sisi sote ni nafsi na kila nafsi itaonja umauti, pumzika kwa amani Dada Nuru Sigera'


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi