MANISPAA YA ILALA YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA.



Na David Langa.
Idara ya elimu msingi ndani ya manispaa ya Ilala imefanya maadhimisho ya siku ya Mazingira kwa shule zote za msingi na Sekondari katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Mecky Sadick aliwaasa watu wote kutunza mzingira bila kusubiri siku ya mazingira kwani suala la mazingira na usafi ni la kudumu na haliwezi kusubiri siku maalum.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyumia muda huo pia kuwataka wakazi wote wa jiji la Dar es salaam pamoja na wageni ote wanaoingia na kutoka kuwa makini na utunzaji wa mazingira pamoja na kutii sheria bila shuruti kwani hatakuwa tayari kuona watu wanavunja sheria ikiwa ni pamoja na wafanya biashara wadogo wadogo kutorudi katika maeneno yaliyokatazwa katika operesheni  ya safisha jiji inayotekelezwa na manispaa zote tatu ambazo ni kinondoni, Ilala na Temeke
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na walimu toka shule za msingi na sekondari ambapowashindi walipewa vyeti, vifaa vya usafi pamoja na pesa taslimu . Mshindi wa jumla ni shule ya msingi  Upanga ambao walikabidhiwa ngao,cheti,vifaa vya usafi pamoja na fedha taslimu shilingi laki tano (500,000) ambayo ilitolewa na ofisi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kama motisha na changamoto kwa shule zingine . shule zingine zilizoshika nafasi kumi za juu ni Minazi mirefu, Maktaba na Bunge.
Zingine ni Uhuru wasichana, Diamond,Olympio,Boma, Msimbazi , Airwing  na Msimbazi mseto. Shule ya iliyoshika nafasi ya nane ni Miembeni, Mnazi Mmoja na namba kumi ni shule ya msingi kimanga.
Idara ya Mazingira ndani ya Manispaa ya Ilala inaongozwa na Afisa Elimu msaidizi Mw. Wema Kajigili chini ya Afisa Elimu Mkuu Mwl Elizabeth Thomas.
Mkuu wa Mkoa akihutubia umati wa wananchi na wanafunzi waliofika katika siku ya mazingira katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar Es salaam


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Mecky Sadick akipokea zawadi toka kwa kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Dr. Severine Asenga.


walimu washindi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi mbali mbali wa Elimu Mkoa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.




Washindi wa kwanza wa Mazingira mwaka 2014 shule ya msingi Upanga wakifurahi pamoja walimu pamoja na wanafunzi wao. aliyeshika taji ni mwal. mkuu wa shule hiyo mw. Paschalia Kinyondo
Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Kinyamwezi nao walizawadiwa cheti pamoja na Ngao ya ushindi katika utunzaji wa mazingira (PICHA ZOTE  NA DAVID LANGA)












Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi