Na David Langa.
Shule ya Msingi na awali ya Heritage iliopo kata ya Kipawa
Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam imeadhimisha miaka kumi tangu
kuanzanishwa kwake mnamo Janauri mwaka 2004.
Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi washule hiyo ambapo
mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa ambaye
aliwakilishwa na Diwani wa kata ya Pugu Mh. Imelda Samjela.
Akisoma Risala kwa mgeni rasmi mkuu wa shule hiyo mwl.
Elijah Apiemi Kebaso alisema shule hiyo ilianzamwaka 2004 ikiwa na wanafunzi 20 na walimu wanne na mpaka sasa shule ina jumla
ya wanafunzi 650 na watumishi 75 wakiwemo walimu na watumishi wasio walimu.
Alisema wanafunzi wa shule hiyo kwa mara ya kwanza walifanya
mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2008 ambapo jumla ya wanafunzi 14
walihitimiu na kufaulu kwa asilimia mia moja na wameendelea kufaulisha kwa
kiwangi hicho ambapo kwa mwaka jana pia wanafunzi 76 walihitimu na kufaulu kwa
asilimia mia moja.
Naye mageni rasmi Mh. Samjela lisema hakutegemea kushuhudia
mafanikio makubwa yaliyofikiwa na shule hiyo kwa kipindi kifupi ikiwa ni pamoja
na kuwa na majengo ya kisasa na kumbi za mikutano mbali mbali na hivyo kuahidi kuwa balozi wa shule hiyo
mahali popote atakapokwenda ndani na nje ya nchi.
Katika mipango ya shule hiyo ya kutimiza miaka kumi ambayo
inatarajiwa kufikia kilele mwezi oktoba mwaka huu 2014 wanatarajia kufanya shughuli mbali mbali za
kijamii ikiwa ni pamoja na kuchangia damu katika benki ya damu ya taifa,
kufanya usafi katika mojawapo ya hospitali hapa jijini, kupanda miti pamoja na
kuwatembelea wagonjwa na watoto yatima. Pia walimuomba mgeni rasmi kuwafikishia
ombi lao kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala na kwa Baraza la Madiwani
kuwapatia moja wapo ya Bustani au mzunguko (round about) ili waweze kuihudumia
kwa kipindi chote cha uwepo wa shule hiyo.
Kwa upande wake kaimu Afisa Elimu msingi Manispaa ya Ilala
Ndg.Hamisi Mlangala alisema ameguswa na ukakamavu na nidhamu iliyojengwa kwa
wanafunzi wa shule hiyo kwa kuona watoto wadogo wakitoa mahubiri fasaha kwa
lugha ya kiingereza mbele ya mgeni rasmi ambapo aliahidi kuwapa ushirikiana wa
karibu huku akizitaka shule zingine pia kuwa na vipindi vya dini katika shule
zao ili kuwajenga watoto wanaomcha Mungu.
Mgeni rasmi, naibu Meya wa Mnispaa ya Ilala Mh. Imelda Samjela akikagua gwaride ya wanafunzi wa shule ya Heritage iliyoandaliwa kwa ajili yake |
Mh. Samjela akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka kumi ya hEritage. |
Kaimu Afisa Elimu idara ya Msingi Mwl. Hamisi Mlangala akitoa neno katika siku ya maadhimisho. |
Mgeni rasmi akipoke zawadi ya mbuzi aliyokabidhiwa na mkuu wa shule ya sekondari Heritage Mw. Fanuel Rhobi |