Na David Langa
Zahanati ya Mvuti
iliopo kata ya Msongola Mnispaa ya Ilala jijini Dar es salaa imeondokana na
adha ya maji baada ya kupata msaada wa kisima kilichochimbwa na Kampuni ya Bia
Tanzania TBL.
Akipokea msaada huo diwani wa kata hiyo Mh. Angelina Malembeka
amesema msaada huo ni wa muhimu na umekuja kwa wakati kwani wananchi wake
walikuwa wanalazimika kubeba ndoo za maji pindi wnapoenda kupata huduma katika
zahanati hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Dr.
Severine Asenga ameishukuru kampuni ya TBL na wafanyakazi wake kwa ujumla wao kwa kuona umuhimu wa kuchangia
huduma za jamii katika Manispaa yake.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa naibu katibu mkuu
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Elias Kwesi ambaye kwa niaba ya Wizara
yake amewataka wananchi wa Mvuti kuwa
walinzi wa Jenereta hiyo ambayo itakuwa inatumika katika kupandisha maji kwenye tanki
ili iweze kudumu.
Jumla ya garama zilizotumika katika uchimbaji pamoja na
ununuzi wa Jenereta ni shilingi Milioni hamsini na saba (57,000,000) ambazo
zimetolewa na kampuni ya Bia, Tanzania Breweries Limited (TBL)
Mgeni rasmi, Naibu Katibu mkuu Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii Dr. Elias Kwesi akikata utepe katika uzinduzi wa Kisima katika zahanati ya Mvuti kata ya Msongola. |
Mgeni Rasmi akimtwisha mmoja wa wakazi wa mvuti kuashiria uzinduzi rasmi wa kisima. |