Na David Langa.
Kamati ya uwekezaji Manispaa ya Ilala chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa wamefanya ziara kutembelea pori la zingiziwa linalotarajiwa kufanyiwa uwekezaji wa utunzaji wa wanyama na misitu (ZOO).
Eneo la zingiziwa lipo ndani ya kata mbili ambazo ni kata za chanika na Msongola likiwa na ukubwa wa hekari 250 ambalo manispaa ya Ilala imeshawalipa wakazi wote na hivyo kupisha uwekezaji huo unaotajiwa kuanza muda wowote kuanzaia sasa.
Akizungumza katika eneo la uwekezaji Mh. Silaa amesema ni vyema wananchi wa wanaozunguka eneo la mradi wakashirikishwa ili wawe sehemu ya umiliki na pia kuongeza ulinzi wa mali ndani ya eneo la mradi.
Kwa upande wake diwani wa kata ya msongola Mh Angelina Malembeka amesema wakazi wa eneo hilo wamepokea mradi huo kwa mikono miwili na ndiyo maana walikuwa tayari kutoa maeneo yao bila tatizo.
|
Mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika ofisia za serikali za mitaa Zingiziwa kabla ya kuanza ziara rasmi. |
|
|
Mkuu wa Kitengo cha mazingira manispaa ya Ilala Ndg Abdon Mapunda akionesha ramani ya eneo la mradi kwa wajumbe waliotembelea eneo la Zingiziwa. |
|
|
Mstahiki Meya akiongoza ziara ndani ya eneo la mradi. |
Mh. Sultan Salim(Mwenyekiti kamati ya mipango miji) akiongozana na wajumbe kupitia mipaka ya eneo la mradi.
|
Msafiri ni kafiri gari likaleta shida hali iliyowabidi wajumbe waanze kusukuma gari wakiongozwa na mstahiki meya Jerry Silaa. |
|
Kazi ikaendelea. |
|
|
Mh. Angwlina Malembeka naye hakuwa nyuma katika zoezi la kusikuma gari na hatimaye safari ikaanza kurudi Ilala. |