Na David Langa
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa amekabidhi jumla
ya madawati 300 zenye thamani ya shilingi Milioni arobaini na tano (45,000,000)
kwa shule tatu za sekondari ndani ya Manispaa ya Ilala.
Shule zilizonufaika na mgawo huo wa mara ya kwanza wa
madawati na idadi ya madawati katika mabano ni Pugu sekondari (107), Jangwani
(100) na Ulongoni sekondari madawati 100.
Hii ni mara ya kwanza
kwa Meya huyo kutoa madawati ikiwa ndani ya programu yake ya MEYORS BALL
iliyozinduliwa mwaka jana ikiwa na lengo la kukusanya jumla ya madawati elfu
thelathini na sita (36,000 ) kwa shule zote za msingi na sekondari ndani ya
manispaa ya Ilala.
Mh. Silaa ambaye pia ni mmoja kati ya wanafunzi waliowahi
kusoma katika shule ya Sekondari ya Pugu aliwataka wadau mbali mbali kuchangia
sekta ya Elimu ambayo ni sekta mama kwa sekta zote za kiuchumi na za kijamii
kote duniani.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo walimu,
madiwani na viongozi toka ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala akiwasili katika viwanja vya shule ya sekondari ya Pugu kwa ajili ya shughuli ya kukabidhi madawati. |
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Pugu pamoja na wenzao wawakilishi toka Shule za sekondari Jangwani pamoja na Ulongoni wakipokea dawati tok kwa Mh. Silaa. |