Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Sera mpya ya elimu ya mwaka 2014, ambapo sera hiyo itaamuandaa Mwanafunzi katika kupambana na changamoto za kiteknolojia na za kiuuchumi ili kuweza kujitengenezea maisha bora hapo baadae
Akizindua Sera hiyo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Majani ya chai iliyopo Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala, Mhe. Rais alisisitiza kuwa "Maisha bora yanawezekana kwa kila Mtanzania kwa kupata fursa ya kupata elimu bora itakayomuwezesha kwenda na wakati na kuyakabili mazingira, hakuna maendeleo bila maendeleo ya elimu"
Katika uzinduzi huo Mhe. Rais pia alipata fursa ya kuzindua Maabara tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Bailojia katika shule ya Sekondari Majani ya chai.
 |
Mhe. Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Taifa katika uzinduzi wa sera mpya ya elimu ya mwaka 2014 katika viwanja vya shule ya sekondari Majani ya Chai |
 |
Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiwasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Majani ya Chai kwa aijili ya uzinduzi wa sera mpya ya elimu ya mwaka 2014. |
 |
Viongozi mbalimbali wakijiandaa kumpokea Mgeni Rais katika uzinduzi wa sera mpya ya elimu ya mwaka 2014. |
 |
Mhe. Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika shule ya sekondari Majani ya Chai kwaajili ya uzinduzi wa Maabara ya masomo ya Fizikia, Baiolojia na Kemia |
 |
Mhe. Rais Jakaya Kikwete akipokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi. |
 |
Mhe. Rais Jakaya Kikwete akizindua Maabara katika shule ya sekondari Majani ya Chai |
 |
Mhe. Rais Jakaya Kikwete akipata ufafanuzi wa matumizi ya vifaa vya maabara kutoka kwa Wanafunzi wa shule ya sekondari Majani ya Chai |