MADIWANI WA MANISPAA YA ILALA WAPITISHA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

Na: Hashim Jumbe
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala limefanya kikao maalum cha mapitio ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2014/2015 na  mapendekezo ya mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 55.9 kutoka vyanzo vyake vya ndani, na shilingi Bilioni 112.3 zinatarajiwa kutoka Serikali Kuu.

Makadirio  ya Matumizi ya Bajeti yanahusisha Kamati ya Fedha na Utawala, Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira na Kamati ya Ukimwi.

Kupitia Kamati ya Mipango Miji na Mazingira imepanga kutumia jumla ya shilingi 14.2 Bilioni kwa ajili ya Mishahara, matumizi ya kawaida ya miradi ya Maendeleo,  Kamati ya Ukimwi inakusudia kutumia jumla ya shilingi Milioni 373.6 kwa ajili ya shughuli za kudhibiti VVU na UKIMWI, Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii imepanga kutumia jumla ya shilingi Bilioni 109.6 kwa ajili ya Mishahara, matumizi ya kawaida ya miradi ya Maendeleo, Kamati ya Fedha na Utawala imepanga kutumia jumla ya shilingi Bilioni 45.1 ikiwa ni Mishahara, matumizi ya kawaida na miradi ya Maendeleo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mhe. Jerry Silaa akiongoza kikao Maalum cha mapitio ya bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2014/2015 na mapendekezo ya  mpango wa bajeti kwa mwaka 2015/2016

Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa mapendekezo ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016


M/kiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala,Mhe. Angelina Malembeka akiwasilisha mbele ya Wajumbe wa Baraza la Madiwani Bajeti ya Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii kwa mwaka 2015/2016
Diwani wa Kata ya Buguruni Mhe. Magina Lufungilo akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wakati wa upitishwaji wa bajeti ya Manispaa ya Ilala kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi