Na David Langa.
Girl guides ni chama cha hiari kinacholenga kuwajengea
watoto wa kike na wasichana uwezo wa kujiamini, kujitegemea, kuitolea na kuwa
na maadili na heshima mbele ya jamii nzima. Nchini Tanzania kuna zaidi ya watoto wa
kike na wasichana zaidi ya laki 2 ambao
ni wanachama hai wa wa chama hiki.
Wiki hii chama hiki kimewaingiza jumla ya wanachama wapya
117 katika shule pekee ya wasichana nchini Tanzania ya Uhuru iliyopo
Manispaa ya Ilala jijini Dar Es Salaam. Wanachama
hawa wapya wamkefikia hatua hiyo baada ya kuhitimu mafunzo ya miezi sita
yaliyokuwa yakiendeshwa na wakufunzi katika shule hiyo ambapo wahitimu
walivyalishwa beji ya uanachama pamoja na kula kiapo cha utii mbele ya mgeni
rasmi.
Moja ya kiapo cha wanachama hao wapya ni kuhakikisha kila
siku kabla ya kulala kutenda jambo moja au zaidi la wema au kujitolea kusaidia
jamii.
Sehemu ya wanachama wapya wa shule ya msingi ya wasichana Uhuru wakisubiri kuapishwa |
Viongozi na walenzi wa chama cha Girls guide wakitoa maelezo kwa wanachama wapya kabla ya kuwaapisha |
Mkufunzi wa kitaifa wa chama hicho Bi. Expencer Violet Siame akiwaapisha wanachama wapya na kuwapa ahadi muhimu za chama . |
Mdhamini wa chama cha Girl guides nchini Tanzania tangu mwaka 1965 Bi.Siami Mohamed akimvisha taji mwanachama mpya baada ya kula kiapo cha utii |