Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala leo imeanza zoezi
la siku mbili la kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa Wananchi wanaoishi katika
Manispaa hiyo, akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa zoezi hilo la
usambazaji wa Katiba hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Claud
Mpelembwa alisema “Manispaa ya Ilala imepokea nakala 10,500 za Katiba inayopendekezwa, na
siku ya leo ya tarehe 24 februari, 2015 tumeanza kuzisambaza kwenye Kata zote
35 za Manispaa ya Ilala na kila Kata itapata nakala 300 kwa ajili ya kuzigawa
kwa Wananchi ambao ni wakazi wa Manispaa
ya Ilala, kwa hiyo tunategemea kila Kaya kupata nakala ya hii Katiba
inayopendekezwa”.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Claud Mpelembwa mwenye suti nyeusi akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa zoezi la ugawanyi wa Katiba iliyopendekezwa. |
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Claud Mpelembwa akiwaonesha Waandishi wa Habari Katiba inayopendekezwa, kabla ya kuanza zoezi la usambazaii kwa Wananchi wa Manispaa ya Ilala. |
Baadhi ya Maafisa wa Manispaa ya Ilala wakijiandaa kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa Wananchi wanaoishi Maispaa ya Ilala.
|