BAPS CHARITIES YAFANYA UKARABATI WA MAJENGO SHULE YA MSINGI MAKTABA

Na: Hashim Jumbe
Taasisi isiyokua ya Kiserikali ya ‘Baps Charities’ imekabidhi majengo ya shule ya msingi Maktaba iliyopo kata ya Upanga Mashariki, Manispaa ya Ilala baada ya kuyafanyia ukarabati mkubwa. Ukarabatit huo ulihusisha vyumba vya madarasa 18 na matundu ya vyoo 20.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Mh. Kassim M. Majaliwa, pia alishuhudia taasisi ya Baps Charities wakikabidhi na vifaa vya kujifunzia kwa kila Mwanafunzi wa shule hiyo ya msingi Maktaba.

Akisoma risala kwa  Mgeni rasmi, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo aliwashukuru Baps Charities kwa msaada wao na aliahidi kuyatunza vizuri majengo hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Mh. Kassim M. Majaliwa mwenye suti nyeusi akimsikiliza Mwanafunzi wa shule ya msingi Maktaba anavyosoma kitabu alipotembelea maktaba ya shuleni hapo

Mh. Kassim M. Majaliwa akimsikiliza Mwanafunzi wa shule ya msingi Maktaba namna ya kuandaa zana za kujifunzia somo la sayansi, alipotembelea banda la maonesho la shule hiyo

Naibu Waziri TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mh. Kassim Majaliwa akizindua rasmi majengo ya shule ya msingi Maktaba yaliyofanyiwa ukarabati na taasisi ya Baps Charities




Kikundi cha utumbuizaji kutoka shule ya msingi Umoja wa Mataifa wakicheza ngoma aina ya makhirikhiri wakati wa hafla hiyo

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Mh. Kassim Majaliwa akimkabidhi mmoja wa Wanafunzi wa shule ya msingi Maktaba vifaa vya kujifunzia kwa niaba ya Wanafunzi wote wa shule hiyo ya msingi Maktaba.


Naibu Waziri Mh. Kassim M. Majaliwa akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa BAPS Swaminaran-dhehebu la dini ya Hindu Bw. Subhash M. Patel 



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi