Na: Hashim Jumbe
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh. Jerry Silaa amewaaga Madaktari sita kutoka Hospitali ya Amana, Kituo cha Afya Chanika na Mratibu wa Mama na Watoto wanaokwenda Korea Kusini kwa ajili ya Mafunzo ya kitaalamu kwenye utabibu.
Mafunzo hayo yanafuatia ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa ya Mama na Mtoto iliyojengwa Kata ya Chanika kwa ufadhili wa KOICA kwa gharama ya shilingi bilioni 6, yatakuwa ya wiki mbili, huku yakitarajia kuwajengea Madaktari hao uwezo wa kutumia vifaa vya kisasa kwa ajili ya kutolea huduma iliyo bora kwa Mama na Mtoto.
Mradi huo wa ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Mama na Mtoto iliyopo Chanika utakuwa na Maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi wa afya ya Mama na Mtoto, vitanda 200, vyumba vya kisasa vya upasuaji na nyumba za Wauguzi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh. Jerry Silaa akiagana na Maratibu wa Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto Dr. Myoung Kim kutoka Korea Kusini
|