HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
|

TANGAZO
MAOMBI YA LESENI ZA VILEO KWA
KIPINDI KINACHOANZIA TAREHE 01 APRIL, 2015 NA KUISHIA TAREHE 30 SEPTEMBA,
2015
Chini
ya Sheria ya Leseni za Vileo Na. 28 ya 1968 na marekebisho yake sehemu 1V
kifungu 38(1) – (4) na 39 (1-3).
Wafanyabiashara wote wanaoendesha
Biashara ya Vileo katika Manispaa ya Ilala wanatangaziwa kwamba Fomu za maombi
ya Leseni za Vileo kwa kipindi kitakachoanza tarehe 01/O4/2015 na kuishia tarehe
30/09/2015 zinaanza kutolewa kuanzia tarehe
16/03/2015.
Fomu za maombi ya Leseni za Vileo
zinapatikana katika Ofisi ya Biashara Manispaa ya Ilala, katika Jengo la
Arnatoglou karibu na Hospitali ya Mnazimmoja.
Fomu za maombi ya zamani (Renewals)
zijazwe kikamilifu na kurejeshwa Ofisi ya Biashara ya Manispaa ya Ilala,
ziambatanishwe na kivuli (Photocopy) cha Leseni ya kipindi kinachoishia tarehe 31/03/2015 pamoja na TIN, pia fomu ipitishwe kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya maendeleo ya Kata husika.
Fomu za maombi mapya zipitishwe
ngazi zote kama zilivyooneshwa kwenye kifungu na 9 (tisa) kabla hazijarejeshwa
katika Ofisi ya Biashara.
Maombi yote yawasilishwe kwa Afisa
Biashara kabla ya tarehe 01/ April, 2015
limetolewa na:-
Isaya M.
Mngurumi
MKURUGENZI
WA MANISPAA
HALMASHAURI
YA MANISPAA YA ILALA.