Na: Hashim Jumbe
Kamati ndogo inayosimamia vibali vya ujenzi Manispaa
ya Ilala ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mh.Sultan Salim, imefanya ziara ya siku
moja ya ukaguzi wa vibali vya ujenzi katika maeneo ya pembezoni mwa mji.
Kamati hiyo ilitembelea eneo la Pugu Kinyamwezi na
kukagua ujenzi wa ghorofa linalojengwa na Kampuni ya KAMAKA na kubaini
mapungufu makubwa katika ujenzi huo ikiwemo kubadilisha matumizi ya kibali cha
ujenzi kutoka kibali cha ujenzi wa ghala la kuhifadhia bidhaa na kutumia kibali
hicho kwa ujenzi wa ghorofa.
Kamati hiyo pia ilitembelea na kukagua ujenzi wa
jengo la hospitali ya kujifunzia kwa vitendo la Chuo kikuu cha Kampala kilichopo
Gongolamboto, na kubaini mapungufu katika ujenzi huo yakiwemo ya kukosekana kwa
kibali cha ujenzi na kibali cha tathmini ya mazingira huku ujenzi huo
ukiendelea kufanyika katika eneo hatarishi.
Kamati hiyo imesimamisha ujenzi wa jengo la KAMAKA na
ujenzi katika Chuo kikuu cha Kampala hadi hapo utaratibu wa ujenzi utakapokua
umefuatwa.
Wajumbe wa Kamati ndogo ya Vibali vya Ujenzi
Manispaa ya Ilala wakifanya ukaguzi katika jengo linalomilikiwa na Kampuni ya
KAMAKA eneo la Pugu Kinyamwezi
|
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Mjumbe
wa Kamati ndogo ya vibali vya ujenzi Mh. Kheri Kessy akiongea na fundi aliyekua
akijenga ghorofa ya KAMAKA
|
Eneo hatarishi kwa ujenzi likiwa limeanza kujengwa
msingi wa jengo la hospitali ya kujifunzia katika chuo Kikuu cha Kampala tawi
la Gongolamboto
|