Na: Hashim Jumbe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo amewatembelea Wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko katika eneo la Buguruni Mnyamani, na kuangalia athari zilizoletwa na mvua hizo kubwa zilizoanza kunyesha tangu ijumaa iliyopita.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete alipata pia fursa ya kuzungumza na Familia zilizoathirika na mafuriko hayo na kuiagiza kamati inayosimamia maafa Mkoa wa Dar-es-Salaam kutoa msaada wa haraka kwa waathirika wa mafuriko hayo pamoja na kuwataka Wananchi hao kuhama katika eneo hilo hatarishi huku Serikali ikijiandaa kuwalipa fidia.
 |
Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa kusimamia maafa ya mkoa Bw. Said Mecky Sadick akimuonesha Rais Kikwete eneo linalotiririka maji yanayotoka kwenye makazi ya Wananchi wa Mnyamani |
 |
Wataalamu mbalimbali wakijitahidi kuondoa maji yaliyoingia katika makazi ya Wananchi wa neo la Mnyamani lililokumbwa na mafuriko |
 |
Rais Kikwete akiangalia namna mafuriko yalivyoathiri nyumba za wakazi wa mtaa wa Mnyamani |