Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekabidhi misaada ya
chakula kwa waathirika wa mafuriko ya Buguruni Mnyamani, ikiwa imepita siku
moja tangu Rais Jakaya Mrisho Kikwete atembelee eneo hilo.
Misaada hiyo ilitolewa kwa kaya 631 zenye Watu 2,650, Watoto chini ya miaka mitano 293, Wazee 62 ilikabidhiwa
kwa Wananchi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ni pamoja na
mchele kilogram 4,500, mafuta ya kupikia lita 10 ndoo 15, huku taasisi binafsi
ya BAPS CHARITIES wakisaidia kutoa mikate na juisi.
Aidha katika zoezi hilo, Mh. Jerry Silaa alitoa wito kwa asasi mbalimbali nazo zijitokeze na kuwasaidia waathirika hao wa mafuriko kwani bado wanahitaji misaada
 |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa wa pili kulia akikabidhi misaada kwa Wananchi wa Buguruni Mnyamani |
 |
Meya Jerry Silaa akiongea na waathirika wa mafuriko ya Buguruni Mnyamani wakati wa kutoa msaada kwa waathirika hao |