Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Shirika la Mazingira Duniani la ‘World
Wide Fund for Nature’ (WWF) limepanda majani aina ya vetiva kwenye kingo za mto
Msimbazi ili kuzuia athari za mmomonyoko wa udongo zinazoweza kusababishwa na
kasi kubwa ya maji yanayotiririka katika mto huo hususani katika vipindi vya
mvua.
Zoezi hilo la upandaji majani katika kingo
za mto Msimbazi, limefanyika katika eneo la Msewe Liwiti kata ya Segerea na
inatarajiwa kupandwa majani katika eneo lenye urefu wa kilomita 25 kwenye kingo za
mto Msimbazi.
Majani hayo yanatabia ya kunyonya sumu
kwenye ardhi, pia yatazuia muendelezo wa mmomonyoko wa kingo kwenye mto
Msimbazi na kupunguza hewa chafu katika maeneo hayo.
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ilala, Ndugu Charles Secha akipanda majani katika kingo za mto Msimbazi eneo la
Misewe kata ya Segerea
|
Maafisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala
wakishiriki zoezi la upandaji majani aina ya vetiva kwenye kingo za mto
Msimbazi
|