Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala anawatangazia wananchi na wakazi wa eneo la
Kariakoo na katikati ya jiji kuwa, zoezi la Usafi wa Mazingira limekuwa
likikwamishwa na magari yanayoegeshwa pembezoni mwa Barabara zote za katikati
ya jiji nyakati za usiku.
Kwa Tangazo hili, Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala inatoa Amri kwa Wakazi wa Eneo la
katikati ya jiji kutokuegesha Magari pembezoni mwa barabara zote kuanzia saa
3.00 usiku.
Halmashauri itachukua hatua ya kuyafunga
magari yote yatakayokutwa yameegeshwa na
Kuyaondoa pembezoni mwa barabara na kuyapeleka Karakana za Halmashauri na
kutakiwa kulipia faini ya Sh.50,000/= kwa kila gari litakalokamatwa na
kulazimika kulipia gharama za kvuta na kulaza gari.
"Manispaa
ya Ilala bila Uchafu Inawezekana"
Limetolewa na,
Isaya
M. Mngurumi
Mkurugenzi
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala