Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Jerry Silaa amezindua ujenzi wa Zahanati katika katika Mtaa wa Mbondole, Kata ya Msongola.
Ujenzi wa Zahanati hiyo utatumia fedha za ndani za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na unatarajiwa kufanyika kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza utatumia kiasi cha Shilingi Milioni Thelathini.
Akiongea na Wananchi wa Msongola, Mhe. Jerry Silaa aliwaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi atakayejenga Zahanati hiyo huku akikemea tabia za wizi wa vifaa vya ujenzi unaofanywa na Wananchi wa maeneo mengine wakati wa shughuli za ujenzi zikiendelea.
Diwani wa Kata ya Msongola, Mhe. Angelina Malembeka akimkabidhi Mwenyekiti wa mtaa wa Mbondole hati za umiliki wa ardhi itakayotumika kwa ujenzi wa Zahanati ya Mbondole |
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akizungumza na Wananchi wa Kata ya Msongola wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Zahanati ya Mbondole |