Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala anapenda kuwatangazia nafasi za kazi
Watanzania wenye sifa kama ifuatavyo:-
1. MTENDAJI WA MTAA III – NAFASI 30
SIFA
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha IV au VI
aliyehitimu Astashahada (CHETI) katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii,
Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI YA MAJUKUMU
i.
Katibu wa Kamati ya Mtaa
ii.
Mtendaji Mkuu wa Mtaa
iii.
Mratibu wa utekelezaji wa
Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
iv.
Mshauri wa Kamati ya Mtaa
kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa
v.
Msimamizi wa Utekelezaji wa
Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa.
vi.
Mshauri wa Kamati ya Mtaa
kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama
vii.
Msimamizi wa utekelezaji wa
mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa;
viii.
Kusimamia ukusanyaji wa
Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote;
ix.
Kuandaa na kutunza rejesta
ya wakazi wote wa Mtaa na
x.
Atawajibika kwa Mtendaji wa
Kata.
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. B
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. B
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II –
NAFASI II – NAFASI 10
SIFA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV/VI wenye cheti cha Utunzaji
Kumbukumbu kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU
Wasaidizi wa kumbukumbu watafanya kazi zifuatazo hapa chini kwa
kuzingatia fani walizosomea na kazi wanazofanya ni kama vile Uhifadhi wa
Nyaraka, Uhifadhi wa Kumbukumbu za Afya, Ardhi na Masjala ya Kawaida,
1 KAZI
YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II
Daraja hili la mafunzo katika kazi, hivyo atafanya kazi kwa maelekezo
ya wasaidizi wa kumbukumbu walio juu yake. Kazi atakazojifunza na kufanya ni
zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu daraja la I.
2. KAZI ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA I
i. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili
yanayohitajiwa na wasomaji
ii. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa
kumbukumbu/nyaraka.
iii.
Kuchambua, kuoredhesha na kupanga
kumbukumbu/nyaraka katika makundi
kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya
matumizi ya ofisi.
iv. Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika
reki (file racks/cabinets) katika
masjala/vyumba vya kuhifadhia
kumbukumbu.
v. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka n.k)
katika mafaili.
vi. Kushughulikia maombi ya
kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. B
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji lazima awe Raia wa
Tanzania
- Awe amehitimu na kupata Cheti cha Taaluma cha Kidato cha Nne (IV)
NB. Results
Slip hazikubaliki.
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa
- Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo:-
i.
Nakala za Vyeti vya Mwombaji
vilivyothibitishwa,
ii.
Maelezo binafsi ya Mwombaji
(Curriculum Vitae),
iii.
Picha ndogo za rangi
(Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji za hivi karibuni.
- Kila Mwombaji lazima awe na Umri kati ya miaka 18 – 45
- Waombaji wenye sifa Pungufu
au Zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauriwi kuomba kwani maombi yao
hayatafanyiwa kazi.
- Watumishi waliopunguza kazi/kufukuzwa kazi Serikali
hawashauriwi kuomba
- Waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitishia barua zao za
maombi kwa waajiri wao wa sasa.
- Barua ambazo hazikuambatishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu
(i–iii) hazitashughulikiwa.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono, zikiwa na anwani kamili ya Mwombaji, pamoja na namba ya
simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA YA ILALA
S. L. P 20950
DAR ES SALAAM.
TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA
MAOMBI:-
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/05/2015 saa 9:30 Alasiri
Tangazo hili linapatikana pia
kwenye Blog ya Manispaa ya Ilala – www.habariilala.blogspot .com
Limetolewa na;
ISAYA M. MNGURUMI
MKURUGENZI
WA MANISPAA,
HALMASHAURI
YA MANISPAA YA ILALA