Na: Hashim Jumbe
Idara ya Elimu Msingi na Elimu Sekondari Manispaa ya
Ilala, wameadhimisha siku ya elimu (Elimu Day) na kufikia kilele cha uboreshaji
wa mazingira kwa Walimu na Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari zilizopo
Manispaa ya Ilala.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika mwishoni mwa juma
lililopita katika viwanja vya Mnazi Mmoja yaliwashirikisha Wadau mbalimbali wa
elimu na mazingira wakiwemo Waratibu wa Clasta, Waratibu wa Elimu Kata, Wakuu
wa Shule na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.
Aidha, maadhimisho hayo yaliambatana na utoaji wa
zawadi mbalimbali zikiwemo vifaa vya usafi, vikombe vya ushindi na vyeti kwa
Walimu na Wanafunzi waliofanya vizuri katika taaluma na usafi wa mazingira.
Akitoa
wito kwa Wananchi
wanaoishi Manispaa ya Ilala pamoja na asasi zote, Idara na sekta za Umma, Mgeni
Rasmi wa Maadhimisho hayo Mh. Raymond Mushi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala
amewataka kuhakikisha suala la Elimu ya Mazingira na Usafi linapewa kipaumbele katika maeneo yao. “Kila mmoja kwa
nafasi yake anatakiwa ashiriki kikamilifu katika kuhifadhi
mazingira kulingana na Sheria
zilizopo zinavyoelekeza. Nasisitiza,
kuwa Maafisa Mazingira na Mabwana Afya
katika ngazi mbali mbali kufanya kazi kwa bidi”.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakiandamana kupita mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya elimu na kilele cha uboreshaji wa mazingira huku wakiwa na bango linalosomeka “Elimu bora, kwa mazingira bora”
|
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Issaya Mngurumi,aliyepo kushoto akimkabidhi Mgeni
Rasmi zawadi iliyotolewa na Walimu kwa kuthamini mchango wake katika sekta ya
elimu
|
Walimu
na Wanafunzi wa shule ya Tusiime wakishangiria ushindi wa jumla walioupata
katika maadhimisho ya siku ya elimu na kilele cha uboreshaji wa mazingira kwa
mwaka 2015.
|
Afisa
Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Bi. Elizabeth Thomas akicheza ngoma aina ya
makhirikhiri pamoja na Wanafunzi kutoka shule ya msingi Umoja kutoka Kiwalani
|