MEYA SILAA AWAAGA WANANCHI WA MANISPAA YA ILALA KWA FUTARI




Na: Hashim Jumbe
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala anayemaliza muda wake wa Uongozi wa kipindi cha mwaka 2010-2015 Mhe. Jerry Silaa amewaaga Viongozi na Wananchi wa Manispaa ya Ilala kwa futari aliyoiandaa kwenye ofisi za Manispaa ya Ilala-Arnatoglou muda mfupi baada ya kulivunja Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo kwa mujibu wa sheria.

Katika hafla hiyo ya futari iliyohudhuriwa pia na Viongozi wa Dini wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, hafla iliongozwa na Dua maalum ya kuliombea Taifa letu liendelee kudumisha amani na kuwatakia kheri Viongozi wetu katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Aidha, Mhe. Jerry Silaa alitumia nafasi hiyo kuwashukuru Watu wote kwa ushirikiano waliokua wakimpa katika kipindi chake cha Uongozi wa Manispaa hiyo na kumuombea kheri kila Mmoja.








Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya Mngurumi akizungumza na Waalikwa katika hafla ya futari
Mhe. Jerry Silaa akizungumza na Wageni waliohudhuria hafla ya futari  
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Alhad Mussa Salum akitoa mawaidha mafupi wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mhe. Jerry Silaa
 
 



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi