BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA ILALA LAMALIZA MUDA WAKE WA UONGOZI



Na: Hashim Jumbe
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala anayemaliza kipindi chake cha Uongozi kwa kipindi cha mwaka 2010-2015 Mhe. Jerry Silaa amelivunja Baraza la Madiwani la Manispaa  hiyo kwa mujibu wa sheria na kama ilivyoagizwa kwenye tangazo la Serikali Namba 230 la tarehe 26 Juni,2015 ambapo Halmashauri zote nchi zimeagizwa kuvunja Mabaraza ya Madiwani kabla ya tarehe 08 Julai, 2015.

Akisoma hotuba ya kuvunja Baraza kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jerry Silaa alisema “Baraza hili la Madiwani la Awamu ya tatu ya Uhai wa Halmashauri linavunjwa likiwa lina mambo ya kujivunia hususani katika kuandaa mazingira endelevu ya Uwekezaji, Kuongezeka kwa mapato ya ndani, Uboreshaji wa huduma za Kiuchumi, elimu na Afya. Nampongeza Mkurugenzi na timu yake ya wataalam, Waheshimiwa Madiwani wote, Uongozi wa Wilaya, Uongozi wa Mkoa na wataalam wake. Ushirikiano wa karibu wa timu hii umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio tunayoyaona kwa sasa. Naamini Awamu ya nne ya Uongozi unaokuja utaanzia mahali pazuri”

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, Alhad Mussa Salum akisoma dua ya kuliombea Baraza la Madiwani na kuwaombea kheri katika Uchaguzi Mkuu ujao





Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe.Yusuph Mwenda Akitoa salamu za Manispaa ya Kinondoni katika wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani

Mhe. Jerry Silaa akihutubia Mkutano wa Baraza la Madiwani muda mfupi kabla ya kulivunja Baraza hilo


Mhe. Jerry Silaa akikabidhiwa bendera ya kumbukumbu ya Manispaa ya Ilala na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya Mngurumi
 


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi