1.0 Utangulizi
Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala inakusudia kuendeleza maeneo 20 ya wazi kwa ubia, na
inakaribisha Wadau wa utunzaji wa Mazingira ili kuingia mkataba wa kuendeleza
maeneo hayo. Maeneo yanayokusudiwa kwa kuanzia yanajumuisha Bustani za
Mapumziko, Maeneo ya Wazi, Mizunguko ya barabara na Barabara kuu sehemu za
katikati na pembeni.
2.0 Orodha ya Maeneo
Mchanganuo
wa maeneo yanayokusudiwa kuendeshwa kwa ubia ni kama ifuatavyo:-
S/N
|
ENEO
|
MAHALI
LILIPO
|
1.
|
Bustani
za Mapumziko
|
i.
Umoja
wa Vijana Eneo la Wazi (Barabara ya Morogoro mkabala na Jengo la Vijana.
ii.
Palm
Beach (Makabala na Palm Beach Hotel)
iii.
Karimjee
Botanical Garden
|
2.
|
Maeneo
ya Wazi
|
i.
Baclays
(Mkabala na Hotel ya Royal Palm)
ii.
Stetesheni
iii.
Viwanja
vya Mnazi Mmoja No. 1 (Mashujaa)
iv.
Viwanja
vya Mnazi Mmoja No. 2 (Ofisi ya Kata Mchafukoge)
v.
Viwanja
vya Mnazi Mmoja No.3 (Viwanja vya Michezo)
vi.
Cocabs
(Eneo la wazi – Makutano ya barabara ya Lumumba na Nyerere)
vii.
Mahakama
ya Kariakoo (Eneo la wazi-Makutano ya barabara ya Lumumba na Morogoro)
viii.
Samora
Mkabala na Benki ya NBC (Barabara ya Samora/ India)
ix.
Mpilipili mkabala na Barabara ya Lithuri
|
3.
|
Mizunguko
ya Barabara
|
i.
Mzunguko
wa Clock tower
ii.
Mzunguko
wa Askari Monument na Eneo la wazi la Askari Monument (Balcon)
|
4.
|
Barabara
|
i.
Barabara
ya Nyerere
ii.
Barabara
ya Kawawa
iii.
Barabara
ya Lumumba
iv.
Barabara
ya Bibi Titi
v.
Barabara
ya Uhuru
vi.
Barabara
ya Sokoine
vii.
Barabara
ya Luthuli
|
3.0 Mashartiya Muombaji
Halmashauri
itachangia eneo la ardhi na itaingia Mkatataba na Muombaji kwa masharti
yafuatayo:-
- Mwombaji atakuwa ni mpangaji wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
- Mwombaji awasilishe maombi ya
eneo analotaka kuendeleza na rasimu ya Mkataba wa uendelezaji kwa
Mkurugenzi ambao utarekebishwa/ utahakikiwa kabla ya kusainiwa.
- Mwombaji abainishe na
kuthibitisha uwezo wake kifedha, nyenzo, wataalamu, uzoefu na uhusiano wa
shughuli zake kwa sasa na jinsi zitakavyochangia kuboresha eneo husika
- Mwombaji hataruhusiwa kujenga jengo
la kudumu au kufanya biashara kinyume na matumizi yaliyokusudiwa kwenye
eneo analoomba.
- Mwombaji aonyeshe manufaa
atakayopata katika usimamizi na uendelezaji wa eneo hilo.
- Baada ya makubaliano na kuingia
mkataba, Halmashauri haitagharamia maeneo hayo katika kipindi cha mkataba.
Maombi
yote yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kabla au
ifikapo tarehe 14.09.2015.
Isaya M. Mngurumi
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA
YA ILALA