WAZIRI KOMBANI ATEMBELEA BANDA LA MANISPAA YA ILALA KWENYE MAONESHO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO

Na: Hashim Jumbe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani amelitembelea banda la Manispaa ya Ilala kwenye maonesho ya nane nane Mjini Morogoro na kujionea bidhaa mbalimbali zinazopatikana Manispaa ya Ilala pamoja na kutembelea katika shamba darasa.

Mhe. Kombani alipata pia fursa ya kuzindua kisima cha maji kitakachotumika kwaajili ya umwagiliaji wa vipando kwa Wakulima na unyweshaji maji kwa mifugo iliyoyopo kwenye banda la Manispaa ya Ilala, na pia alijionea namna ya samaki aina ya perege wanavyoweza kupandikizwa mayai ya uzazi na kupata watoto.

Mhe. Celina Kombani akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na Wajasiriamali toka Manispaa ya Ilala


Afisa Uvuvi Manispaa ya Ilala, Ndugu Msongo Songoro akionesha namna ya kupandikiza mayai kwa samaki aina ya perege kwa njia ya kitaalam





Waziri Kombani akizindua kisima cha maji kwaajili ya umwagiliaji wa vipando na kunyweshea mifugo



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi