Na: Hashim Jumbe
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa sehemu ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mh. George Simbachawene amefanya ziara katika soko la Buguruni na kujionea hali ya usafi katika soko hilo, uendeshwaji wa soko na namna ya ukusanywaji wa mapato unavyofanyika katika soko hilo.
Katika ziara hiyo, Mh. Simbachawene alijionea changamoto zinazowakabili Wafanyabiashara wa soko hilo, ikiwa ni pamoja na ukosekanaji wa miundombinu rafiki kwa vipindi vyote vya mvua na jua.
Aidha, Waziri Simbachawene aliagiza kufanyika kwa jitihada za makusudi za kuboresha hali ya miundombinu iliyopo sokoni hapo, na pia kufanyike maboresho kwenye ukusanyaji wa mapato sokoni hapo ikiwa ni pamoja na utumiaji wa njia za kieletroniki zitakazosaidia kuongezeka kwa mapato sokoni hapo.
|
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh. Raymond Mushi akimkaribisha sokoni Buguruni Mh. Simbachawene,alipofanya ziara sokoni hapo leo asubuhi. |
|
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Isaya Mngurumi akifafanua namna Manispaa inavyokusanya mapato kwenye soko la Buguruni |
|
Waziri Simbachawene akikagua hali ya usafi kwenye soko la Buguruni |
|
Waziri Simbachawene akiongea na Wafanyabiashara wa soko la Buguruni alipofanya ziara leo asubuhi
|