MANISPAA YA ILALA WAKABIDHIWA JENGO LA KITUO CHA MNAZI MKINDA BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI NA CHESS FOUNDATION

Na: Hashim Jumbe

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Isaya Mngurumi leo amekabidhiwa jengo la kituo cha Mnazi Mkinda baada ya kukamilika ukarabati uliofanywa na 'Chess Foundation'.

Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi, Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Elizabeth Thomas alisema "Tunapenda kusema kuwa kukamilika ukarabati huu, mtakuwa mmehimiza mchakato uliopo katika programu yaMnazi Mkinda wa kuibua na kuviendeleza vipaji vya Watoto katika fani za taaluma,michezo na sanaa."

Mnazi Mkinda ni mpango  mkakati unaolenga kumjengea Mwanafunzi uwezo wa 'KUJITAMBUA', 'KUJIAMINI', na 'KUJITEGEMEA'. Uwepo wa kituo cha Mnazi Mkinda utawezesha kukusanya pamoja Wanafunzi waliojitokeza kwenye fani mbalimbali ili kuwapa maelekezo ya pamoja kuhusiana na fani zao.
Mwenyekiti wa Chess Foundation, Bwana Vinay Choudary akifungua mlango wa jengo la kituo cha Mnazi Mkinda kama ishara ya kuanza kutumika rasmi kwa jengo hilo

Walimu Wakuu kutoka shule za Clasta ya Gerezani wakishuhudia makabidhiano ya jengo la kituo cha Mnazi Mkinda kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mnazi Mmoja


Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala, Bi. Elizabeth Thomas akimuonesha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya Mngurumi wa kwanza kulia vyumba vilivyopo kwenye jengo la Mnazi Mkinda 


Muonekano wa jengo la kituo cha Mnazi Mkinda baada ya kufanyiwa ukarabati na Chess Foundation





Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi