Na:
Hashim Jumbe
Kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani Manispaa ya
Ilala kimepokea na kuipitisha taarifa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa hiyo kuhusu kumbukumbu ya maamuzi ya utekelezaji wa
shughuli za Halmashauri zilizofanyika katika kipindi ambacho Baraza la Madiwani lilivunjwa.
Aidha, kikao hicho kiliambatana na uchaguzi wa
Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri, ambapo nafasi ya Mwenyekiti wa
Kamati ya Mipangomiji na Mazingira ilikwenda kwa Mh. Kassim Msham, na nafasi ya
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii ilichukuliwa na Mh. Greyson
Siwila.
Uchaguzi mwengine ulikuwa ni kwenye Kamati ya
Maadili, ambapo Mwenyekiti wake amekuwa ni Mh. Wilson Mollel.
Kamati nyengine ya Fedha na Utawala Mwenyekiti wake
anakuwa ni Mstahiki Meya kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza na ile Kamati ya
Ukimwi nafasi ya Mwenyekiti inakwenda kwa Naibu Meya.
Wajumbe wa Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Manispaa |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh. Charles Kuyeko akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani. |