Na: George Mwakyembe
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh. Charles Kuyeko amefanya ziara katika machinjio ya Mazizini kata ya Ukonga na kupokea kero mbalimbali kutoka kwa Wamiliki na Watumiaji wa machinjio hayo.
Akiongea na Wamiliki wa machinjio hayo ya Mazizini, Mstahiki Meya Kuyeko aliwaagiza Wamiliki kuhakikisha machinjio hayo yanasajiliwa, pia aliwaagiza kuwa na kumbukumbu ya idadi ya ng'ombe wanaochinjwa kwa siku kwenye machinjio hayo, na mwisho aliwaagiza kusimamia usafi kwenye upatikanaji wa huduma hiyo na kufanya marekebisho sehemu hiyo ya machinjio

Afisa Biashara machinjio ya Mazizini Ndugu Alpha George wa nne kushoto akielezea changamoto zilizopo kwenye machinjio ya mazizini wakati wa ziara ya Mstahiki Meya kwenye machinjio hayo ya Mazizini |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh. Charles Kuyeko akitoa maagizo kwa Wamiliki wa machinjio ya Mazizini |