Na Tabu Shaibu
Katika kuhakikisha kuwa Serikali
inaendelea kutoa huduma kwa kadri ya matarajio ya wengi tarehe 15/02/2016 Mhe.
Selemani Jaffo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
alifanya ziara katika Soko la Samaki Feri.
Katika Ziara yake Mhe. Jaffo alitoa
maelekezo kwa Uongozi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha kuwa kero zilizopo
katika soko hilo zinatatuliwa ndani ya kipindi cha Mwezi Mmoja kwani aliahidi
kurudi sokoni hapo tarehe 15/03/2016 kufuatilia utekelezaji huo.
Miongoni mwa kero ya muda mrefu
iliyokuwepo ni kukosekana kwa Bodi ya Soko suala ambalo alihakikishiwa na
Uongozi wa Manispaa kutatuliwa ndani ya muda huo kufuatia kuidhinishwa kwa
matumizi ya Sheria ndogo za Soko za
Uendeshaji wa Soko la Samaki Feri.
Kwa upande wa mapato Mhe. Naibu
Waziri aliagiza kuwa kila eneo la ukusanyaji sokoni hapo litumie mashine za
kielektroniki na kueleza kwamba Soko la Samaki Feri ni mojawapo ya chanzo cha
mapato kinachotegemewa.
Aidha alipongeza jitihada
zinazochukuliwa za kuliweka soko katika Hali ya Usafi. Maagizo mengine
aliyoyatoa ni pamoja na kurekebishwa kwa Chemba ya maji taka na kuanza kufanya
kazi kwa majiko yatakayotumia mfumo wa gesi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Isaya Mngurumi wa tatu kutoka kulia akitoa maelezo kuhusiana na majiko mapya ya kukaangia samaki yatakayotumia mfumo wa gesi soko la samaki feri |
Naibu Waziri TAMISEMI, Mh. Selemani Jaffo akisalimiana na Wakaanga samaki sokoni feri wakati wa ziara ya kukagua majiko mapya ya kukaangia samaki yatakayotumia mfumo wa gesi |
Mdau wa soko la samaki feri kutoka zone namba nane akimueleza Naibu Waziri Jaffo changamoto za wafanyabiashara ndogo ndogo wanaopanga bidhaa nje ya soko |
Naibu Waziri TAMISEMI, Seleman Jaffo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Ndugu Isaya Mngurumi juu ya uendeshaji wa soko |