Na: Hashim Jumbe
Baraza
la Madiwani la Manispaa ya Ilala limepokea na kuipitisha taarifa ya Hesabu za
Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/2016 katika kikao maalum cha Baraza hilo
kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Arnatouglou.
Akiwasilisha
taarifa ya hesabu za mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha ulioisha tarehe
30-6-2016, Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala, Bw. Mohamed Mkwawa alisema “ili
kukidhi matakwa ya uwasilishaji wa Hesabu za mwisho za Halmashauri kabla ya
kuwasilishwa kwa Wakaguzi wa Nje, ni lazima zipitishwe kwenye Menejimenti,
Kamati ya Fedha na Utawala, na hatimaye kwenye Baraza la Madiwani”
Bw.
Mkwawa aliendelea kusema “Hesabu hizi zimekwishajadiliwa kwenye Kikao cha
Menejimenti, Kamati ya Fedha na Utawala na sasa inawasilishwa kwenye Kikao cha
Baraza la Madiwani kabla ya kupelekwa
kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama sheria inavyotaka”
Kikao
cha Baraza la Madiwani kiliipokea taarifa hiyo na kujadiliana kwa kina na kisha
wote kwa pamoja wakaridhia taarifa hiyo na kuipitisha kwa pamoja.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh. Charles Kuyeko akifungua kikao maalum cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea,kujadili na kuipitisha taarifa ya hesabu za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/201 6 |
Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala, Bw. Mohamed Mkwawa akiwasilisha taarifa ya hesabu za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/2016 |