Na
Neema Njau
Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala yawataka Wamiliki wa Mabango kulipia kodi ya Mabango kwa
wakati ili kuweza kutimiza adhima ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya
Maendeleo.
Akiongea na Waandishi
wa Habari jana Habari Maelezo, Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bibi Tabu
Shaibu alieleza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inaendesha zoezi la
kuyaondoa mabango ambayo hayajalipiwa ushuru kwakuwa wamiliki wa Mabango hayo walishataarifiwa
kulipa Madeni yao, lakini bado wapo baadhi ambao wamekaidi agizo hilo.
Alieleza kuwa ni
vyema wamiliki wa Mabango kufuata utaratibu za uwekaji wa mabango ikiwa ni
pamoja na Mhusika wa bango kupeleka maombi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
ili apatiwe kibali cha kuweka bango, na kupewa taratibu za kulipia bango kila
Mwaka , pamoja na maelekezo ya kuwepo kwa Stickers katika kila bango
zinazoonyesha anuani na jina la Mmiliki wa Tangazo.