IDARA YA ELIMU MSINGI MANISPAA YA ILALA WAJIFANYIA TATHMINI KWA MWAKA 2016

Na: Hashim Jumbe
Ni mwaka wa nne sasa tangu Idara ya Elimu Msingi-Manispaa ya Ilala wajiwekee utaratibu wa kujifanyia tathmini inayowasaidia kutambua changamoto na mafanikio waliyokabiliana nayo kwenye mwaka husika ambapo kupitia tathmini hiyo wataweza kujisahihisha na kuongeza jitihada kwenye mwaka unaofuata ili kufikia malengo yao ya kuiboresha sekta ya Elimu kwa Manispaa ya Ilala.

Katika tathmini iliyofanywa kwa mwaka huu wa 2016, Idara hiyo imepata changamoto kubwa ya kushuka kwa ufaulu kwa Wanafunzi waliomaliza elimu ya darasa la saba kwa mwaka 2016 ukilinganisha na miaka mingine ilivyokuwa.

Aidha, katika tathmini hiyo Watumishi wa Idara ya Elimu Msingi waliofanya vizuri zaidi walipewa motisha mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutunikiwa vyeti na zawadi nyengine mbalimbali.

Tathmini hiyo ilifuatiwa na tafrija fupi kama sehemu ya kupongezana kwa kufanya kazi kwa mwaka mzima na kutakiana kheri kwa mwaka unaokuja.



























Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi