Na: Hashim Jumbe
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Msongela Nitu Palela amefungua semina ya mafunzo ya uandaaji wa bajeti kwa kutumia dhana ya fursa na vikwazo vya maendeleo kwa timu ya mpango shirikishi.
Timu hiyo inawajumuisha Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo wa Kata na Wajumbe wa mpango shirikishi, huku mafunzo hayo yakitolewa kwa mgawanyo wa Majimbo matatu ya Manispaa ya Ilala ambayo ni Segerea, Ilala na Ukonga.
Mafunzo hayo yanalenga kwenye kuwajengea uwezo timu ya mpango shirikishi waweze kupata mbinu zitakazowasaidia kwenye uibuaji wa vipaumbele vya Mitaa na Kata kutoka ngazi ya Wananchi kuvileta kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata na baadae kuwasilisha kwa Mkurugenzi kupitia Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ili kufanyia majumuisho na miradi mingine ya Halmashauri na kufikisha mapendekezo hayo kwenye Kamati za Kudumu za Halmashauri

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Bw. Msongela Palela akifungua semina ya mafunzo ya uandaaji wa bajeti |